The House of Favourite Newspapers

Baba Agoma Kumzungumzia Kichuya

Mchezaji wa Simba, Shiza Kichuya

LICHA ya kikosi cha Simba kuonekana kimesheheni wachezaji wengi msimu huu baba mzazi wa mchezaji wa Simba, Shiza Kichuya amesisitiza kuwa bado anampa muda.

 

Msimu uliopita, Kichuya licha ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa mchezaji ambaye alitoa pasi 20 za mabao na kuwa mmoja ya wachezaji wa kikosi bora cha ligi kuu.

 

Kichuya msimu uliopita alifunga mabao saba huku akicheza mechi nyingi zaidi na akiwa mpishi mkuu wa mabao ya Simba ambayo yalifungwa jumla ya mabao 62.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ramadhani Kichuya ambaye ni Baba wa mchezaji huyo anaamini kuwa mwanaye anahitaji muda kwa sasa ndipo aweze kuzungumzia kiwango chake kwa msimu huu ambao ndiyo kwanza unaanza.

 

“Unajua msimu ndiyo kwanza unaanza na Simba imecheza mechi mbili na safari hii Simba ina wachezaji wengi kweli lakini Kichuya anabaki kuwa bora lakini kiwango alichoonyesha msimu uliopita ukisema niseme sasa kuwa msimu atakuwa hivyo nitakuwa muongo ngoja tumpe muda kwanza acheze mechi nyingi kwanza hapa ndipo taweza kusema lolote.

 

“Lakini timu yao kwa ujumla jinsi ilivyo ina uwezo wa kufika mbali kikubwa tu wao najua wamejiwekea malengo yao hivyo wanaweza kufanya makubwa tena msimu huu,”alisema Baba Kichuya.

Comments are closed.