The House of Favourite Newspapers

Makelele: Mourinho Kachoka

Jose Mourinho

KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Claude Makelele amedai kuwa anaamini kocha wake wa zamani, Jose Mourinho amecho-shwa na mwen-delezo wa kukuza vipaji ndani ya Manchester United.

 

Makelele alikuwa nguzo muhimu enzi zake akiwa chini ya kocha huyo kwenye kikosi cha Chelsea, amesema kuwa kizazi cha sasa na kile chao vina utofauti mkubwa wa uelewa na aina ya uchezaji.

 

Mourinho amekuwa katika presha kubwa kikosini kwake kutokana na matokeo mabaya huku mara kadhaa akikwaruzana na wachezaji wake klabuni hapo.

 

“Alipokuwa Chelsea alikuwa na wachezaji waliokomaa kama mimi, John Terry na Frank Lampard. Kwa sasa hali ni tofauti.

 

“Anachoka kutokana na kinachoendelea, amefundisha vizazi tofauti na vyote vimekuwa na tabia tofauti pia, nahisi anakosa tabia kama ya kile kizazi chetu japokuwa bado anafanya kazi kwa bidii,” alisema Makelele.

 

Baadhi ya wachezaji wake wa United ambao wamekwaruzana na Mourinho ni Eric Bailly na Paul Pogba.

Pogba, alijiunga klabuni hapo akitokea Juventus miaka miwili iliyopita kwa pauni 89m lakini amekuwa akihusishwa kuondoka kwenda Barcelona na Juventus.

 

Kitendo cha kufungwa michezo miwili dhidi ya Brighton na Tottenham kiliongeza presha ya kocha huyo kufukuzwa huku Zinedine Zidane akitajwa kuwa tayari kuchukua nafasi yake.

Comments are closed.