The House of Favourite Newspapers

Shabiki wa Yanga, Real Madrid atwaa Milioni 70.7 za M-Bet

Ofisa habari  wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (kushoto) akimkabidhi, Given Nasson (30) hundi ya Mil. 70, 717,920  ambazo amejishindia.

 

Mkazi wa Kagera, Given Nasson Mgale (30) ameshinda Sh.70, 717,920 kwa kubashiri kiusahihi Mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet.

 

Given ambaye  alisema kuwa yeye ni shabiki wa timu za Yanga, Real Madrid na Manchester United amekuwa mshindi wa 11 wa droo hiyo ambayo mshindi anatakiwa kubashiri kiusahihi si chini ya mechi 12 ya ligi mbalimbali duniani.

 

 

Msemaji wa Kampuni ya M-Bet, David Malley alisema kuwa M-Bet inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kubadilisha maisha mbalimbali ya watanzania. Malley alisema kuwa serikali imejipatia Sh14 millioni ikiwa ni kodi ya asilimia 20.

 

 

“Given anaungana na washindi wengine 10 ambao mpaka sasa wamejishindia mamilioni ya fedha na kubadili maisha yao. M-Bet tunajivunia kuwa kampuni pekee ambayo mpaka sasa imewafaidisha watu wengi kupitia michezo yake, naomba Watanzania kuendelea kubashiri na kampuni michezo yetu kwa njia ya mitandao, simu ya mkononi na mengineyo,” alisema Malley.

 

 

Kwa upande wake, Given alisema kuwa alicheza michezo  104 ya M-Bet kwa kutumia Sh 1,000 na kubahatika kushinda droo iliyofikia tamati Septemba 17. Alisema kuwa alipopigiwa simu na Meneja Masoko wa M-Bet, hakuamini kwani siku hiyo alikuwa hajausoma ubashiri wake.

 

 

“Nilikuwa nipo kazini, nilipokea simu na kuambiwa kuwa nimeshinda, sikuamini, nilipoambiwa nisafiri mpaka Dar es Salaam na leo kupokea fedha zangu, ndipo nimeamini ndoto yangu,” alisema Given.

 

 

Alisema kuwa atatumia fedha hizo kujenga nyumba mbili mkoani Dodoma ambazo moja itakuwa ya kwake na nyingine kwa ajili ya wazazi wake.

 

 

“Pia nitatumia fedha hizi kusomesha watoto wangu na kusaidia ndugu zangu, kwa kweli ndoto zangu zimetimia na sitaacha kubashiri kwa kupitia M-Bet, mechi wamazoweka kwa ajili ya kubashiri ni rahisi na zinaeleweka,” alisema.

 

Comments are closed.