The House of Favourite Newspapers

WAZIRI ULEGA ATOA POLE KWA WALIOZAMA MWANZA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza jambo.
…Waziri Abdallah Ulega, akiendelea kuzungumza jambo.
Meza kuu ilivyoonekana.
Baadhi ya waumini wa kiislamu wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Taswira ilivyoonekana ukumbini hapo.

 

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, ametoa salamu za pole kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajali mbaya iliyotokea mkoani Mwanza ya meli ya MV Nyerere iliyozama katika kisiwa cha Ukerewe, ambapo mbali na salamu za pole pia amewatakia Waislam kheri na Baraka njema katika kutimiza mwaka mpya wa kiislam.

 

 

Abdallah Ulege amekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Rais mstaafu Mzee Mwinyi ambaye ndiye alitakiwa kuwa mgeni rasmi. Katika hafla hiyo Maalum ya kutimiza mwaka mpya wa kiislam pia waumini wa kiislam wameomba dua maalum ya kuwaombea marehemu wote waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na hasa viongozi wa dini hiyo wakisisitiza amani na upendo miongoni mwa Watanzania wote bila kubagua dini yoyote.

 

 

Kwa upande wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa amekazia maneno ya rais ya kuwataka wahusika wa vyombo mbalimbali vya usafiri kuzingatia sheria pasipokukiuka ili kuweza kuzuia ajali zisizokuwa za lazima akiwataka wale wote waliosababisha uzembe wa kwenye kivuko hicho kuchukuliwa hatua stahiki.

Comments are closed.