The House of Favourite Newspapers

Kibadeni: Makambo Hamfikii Kagere

Heritier Makambo wa Yanga.

GWIJI wa soka wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema kuwa anaamini Meddie Kagere wa Simba ana nafasi ya kufanya vizuri kuliko Heritier Makambo wa Yanga kwenye mechi ya watani wa jadi Jumapili.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kibadeni amesema kuwa anaamini Kagere ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri kuliko Makambo kwenye mch­ezo utakapigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Meddie Kagere.

“Tunachoki­tazama kutoka kwa mtu ni nafasi yake, tunaangalia jinsi gani ana uwezo wa kutumia nafasi uwanjani, nafikiri Kagere anaweza kufanya vizuri Jumapili kuliko Makam­bo,” alisema Kibadeni.

Comments are closed.