The House of Favourite Newspapers

Tambwe, Makambo Wahenyeshwa Balaa Yanga SC

Amissi Tambwe (katikati) akishangilia.

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe, jana Alhamisi aliionja joto ya jiwe kutoka kwa kocha wake, Mwinyi Zahera ambaye alimuhenyesha kwa dakika 45 likiwa ni zoezi maalum la kumfanya arudi kwenye makali yake.

 

Tambwe pamoja na straika mwenzake, Heritier Makambo walifanyishwa mazoezi ya peke yao kwa kukimbia uwanja wa mita 100 kwa zaidi ya dakika 45 sambamba na kuruka koni ikiwa ni maandalizi ya pambano lao la Jumapili hii dhidi ya Simba.

 

Yanga walifanya mazoezi hayo ikiwa ni maandalizi maalum ya kujiandaa dhidi ya Simba katika mchezo ambao watacheza keshokutwa Jumapili.

 

Mazoezi hayo yalifanyika jana Alhamisi kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia mkoani hapa. Katika mazoezi hayo ambayo yalishuhudiwa mubashara na Championi Ijumaa, liliwashuhudia Zahera akiwafanyisha mazoezi ya peke yao Makambo na Tambwe kukimbia na ya kujenga stamina kwa kuruka koni na kufunga kwa kutumia nafasi wanazotengenezewa.

 

Mara baada ya mazoezi hayo, Zahera aliliambia Championi kuwa: “Kama unavyojua Tambwe ndiyo amerejea hivi karibuni kutoka kwenye majeraha, hivyo anahitaji muda zaidi awe sawa na kurudi kwenye kiwango chake ndiyo maana umeona nimewafanyisha mazoezi ya peke yao yeye na Makambo na baada ya muda basi atakuwa vizuri.”

Comments are closed.