The House of Favourite Newspapers

NMB YAFANYA KONGAMANO LA MAWAKALA WAKE

Wakipokea vyeti washiriki.

BENKI ya NMB leo imefanya kongamano la mafunzo kwa mawakala mbalimbali wanaotoa huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo, lengo likiwa ni kuboresha huduma zake na kuwajengea uwezo wa kibiashara mawakala hao.

 

 

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika Sinza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema benki hiyo itaendelea kuwajengea uwezo mawakala hao kwani wao ni sehemu ya benki hivyo huduma zao zinatakiwa kufafana na zinazotolewa kwenye matawi yao.

Aliwataka kuendeleaa kutoa huduma kwa uaminifu kwa wateja na kuzingatia taraatibu walizopewa na Benki ili wateja wanaowahudumia waendelee kuiamini benki yao. Aliongeza NMB itaendelea kuboresha huduma zake na kuendelea kuwa kinara katika sekta ya fedha nchini.

 

 

Katika kongamano hilo la kuwajengea uwezo mawakala wa NMB ikiwa ni muendelezo wa semina hizo nchi nzima, NMB imetoa zawadi na vyeti kwa mawakala wanaofanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya.

Akitoa mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi wa NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia kiufanisi zaidi.

Aidha aliongeza kuwa malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.

Naye, Meneja wa NMB Wakala Kanda ya Dar es Salaam, Kisamo Edwin aliongeza kuwa miongoni mwa matarajio ya NMB hapo baadaye ni kuleta mashine mpya za kisasa kwa mawakala zitakazo kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma na kumuongezea kipato.

 

Comments are closed.