The House of Favourite Newspapers

Beki Mpya Simba Aitaja Yanga

Beki mpya wa Simba, Muivory Coast, Zana Oumar Coulibaly.

 

BAADA ya ku­tua nchini, beki mpya wa Simba, Muivory Coast, Zana Oumar Coulibaly amesema hawafahamu watani wao Yanga huku akiingia hofu ya ubora wa wachezaji wanaounda kikosi hicho.

Beki huyo alitua nchini juzi Jumatano saa 11 jioni akitokea nyumbani kwao Ivory Coast ambaye alitua nchini kwa ajili ya kusajiliwa katika usajili huu wa dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.

 

Simba inataka kumsajili beki huyo kwa ajili ya kuziba nafasi ya Shomary Kapombe ambaye alivunjika kifundo cha mguu na kufanyiwa operesheni nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Championi Iju­maa, Coulibaly alisema anaihesh­imu Yanga kutokana na ukubwa wa klabu hiyo huku akiamini siku atakayokutana nayo mchezo utakuwa na upinzani mkubwa.

Coulibaly alisema, upinzani uta­tokana na ubora wa Yanga ambao anaamini ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, hivyo anausubiria mchezo huo wa mzun­guko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

 

“Mimi siifahamu Yanga, lakini kuanzia hivi sasa nitaanza kui­fuatilia kwa ukaribu baada ya kupata taarifa kuwa ndiyo wapin­zani wakubwa wa Simba, hivyo ni lazima niwajue.

 

“Ninaamini Yanga ni timu bora yenye wachezaji wazuri na kazi kubwa itakuwepo mara nitaka­pokutana nao, mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na upinzani utakaokuwepo.

“Nimepanga kuanza kuifuatilia hivi sasa Yanga baada ya kujiunga na Simba na nitaiangalia kwa kupi­tia mechi za hivi karibuni ambazo imezicheza,” alisema Coulibaly.

Comments are closed.