The House of Favourite Newspapers

Zari Afunguka Kuupokea Mwaka Mpya 2019

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

MFANYABIASHARA Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye pia ni mzazi mwenziye na Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kuupokea mwaka 2019, kwa vile miaka miwili ya 2017 na 2018, alipitia matatizo makubwa likiwamo la kuondokewa na mama yake mzazi.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake, Ivan.

 

Pia, alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujenga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia.  Anasema alijijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

 

“Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.   Asante, nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018,” aliandikaa Zari.

 

Ujumbe halisi aliouandika ni ufuatao:

“2017 i was shattered in ways i could never explain, 2 major deaths of my loved ones, infidelity and other things. 2018 was all about picking up my broken pieces and rebuilding. 2019 am simply ready for a new beginning….

“In life, we hurt, we make mistakes, we forgive, we move on. But, most of all & through it all we learn. Thank You 2018, i still have my breath. #Grateful #Blessed #Thankful Share with me your life story of 2018….,” -ZARI

Comments are closed.