The House of Favourite Newspapers

Gigy: Nampenda MO J, Hatuachani Kirahisi

Gift Stanford ‘Gigy Money’ akiwa na mzazi mwenzake MO J.

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ baada ya kukaa mbali na mzazi mwenzake MO J huku wakidaiwa kumwagana jumla, Gigy ameibuka na kudai kuwa anampenda sana mzazi mwenzake huyo na hawezi kuachana naye kirahisi.

 

Akipiga stori na Showbiz, Gigy alisema siyo rahisi kuachana na MO J kama ambavyo watu wanadhani na hiyo inatokana na penzi la dhati lililopo kati yao.

“Nampenda sana MO J, siwezi kumuacha kirahisi, isitoshe yule ni ababa wa mtoto wangu, mwisho wa siku Mayra anahitaji malezi ya pande zote mbili, kuhusu kugombana kwetu kila siku hilo ni jambo la kawaida tu kwa sababu hata vikombe kabatini huwa vinagongana,’’ alisema Gigy.

STORI NA IMELDA MTEMA

Comments are closed.