The House of Favourite Newspapers

Coastal Yatuma Salamu za Pole Kwa Ali Kiba

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union umetuma salamu za rambirambi kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Ally Saleh Kiba ‘Ali Kiba’baada ya kufiwa na baba yake mzazi.

Ali Kiba ambaye pia ni msanii maarufu, amefiwa na baba yake mzazi, mzee Salehe ambaye alifikwa na umauti jana Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

 

Ali Kiba ni mmoja wa wachezaji wa Coastal Unio ambapo alijiunga mwanzoni mwa msimu huu huku akiendelea pia na shughuli zake za muziki. Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo, Hafidhi Kido imeeleza wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatoa pole kwa mchezaji huyo kutokana na msiba huo.

 

“Tunajua Ali Kiba anapitia katika wakati mgumu kwa sasa mchezaji wetu na sisi tunamfariji na kusema msiba ni wetu sote.

 

“Ni mshituko mkubwa kupoteza mzazi na hauvumiliki lakini Mungu ana makusudi yake kwa kilichotokea, hivyo tunatoa pole kwa ndugu yetu Ali Kiba pamoja na familia yake kwa jumla,” alisema Hafidhi.

Na Martha Mboma

Comments are closed.