DTB YATWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA KIKAPU
Wachezaji wa kikapu kutoka DTB Tanzania wameifunga NMB kwa pointi 90-73 katika pambano la fainali ya michuano ya Kikapu kwa Taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Fainali ya pambano hilo ilifanyika Januari 19, 2019 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam. DTB-Tanzania wamechukua ubingwa huo bila kupoteza mchezo hata mmoja. Benki zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NMB.
Comments are closed.