The House of Favourite Newspapers

Mashabiki kiduchu kuingia uwanjani Al Ahly vs Simba

CHAMA cha Soka cha Misri (EFA) kimetangaza kuwa kimehakikishiwa ulinzi kwa mashabiki wasiozidi 10,000 ambao watahudhuria mchezo wa Al Ahly dhidi ya Simba, kesho Jumamosi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Al Ahly inaongoza Kundi D katika michuano hiyo ikiwa na pointi nne wakati Simba in­ashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi tatu.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuku­tana kwenye Uwanja wa Borg El Arab unaoingiza watu 80,000 waliokaa kwenye siti.

 

Taarifa hizo zimekuja baada ya kutolewa tetesi juu ya idadi ya mashabiki ambao wanatakiwa kuingia uwanjani, hivyo Al Ahly wametakiwa kutoa idadi hiyo ya tiketi ili kukwepa adhabu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na suala la kiusalama.

 

Mwamuzi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Maguette Ndiaye raia wa Senegal na atasaidiwa na Djibril Camara pamoja na El Hadji Malick Samba, wakati ofisa wa nne ni Daouda Gueye.

 

Siku chache zilizopita, Caf ilitangaza kuiondoa Ismaily ya Misri katika michuano hiyo kutokana na mashabiki wao kuonyesha utovu wa nidhamu uliovuka mipaka ikiwemo kurusha mawe uwanjani, chupa za maji, kwa mwamuzi wa akiba na kwa mashabiki wageni katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Club Africain, Januari 18, mwaka huu.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

 

Comments are closed.