The House of Favourite Newspapers

Sababu za Chirwa Kusaini Azam Hizi Hapa

OBREY Chirwa alitikisa kiberiti kwa kugoma kusaini mkataba mpya na Azam FC sasa mabosi hao juzi waliweka kwenye listi jina lake kati ya wachezaji nane ambao hawatokuwa nao msimu ujao, kuona hivyo jamaa akajiwahi na jana kasaini mkataba wa mwaka mmoja.

 

Azam ipo kwenye maandalizi makali ya Kombe la Kagame litakaloanza Julai mwaka huu, pia itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao. Mshambuliaji huyo Mzambia, tayari ameripoti katika timu hiyo na kuanza mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Kagame.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd alisema kuwa, Chirwa amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea timu hiyo baada ya kufikia makubaliano mazuri.

 

Jaffar alisema, awali walikuwa wanavutana kwenye dau la usajili ambalo alilokuwa analihitaji yeye kabla ya kugoma na baadaye kutangaza kumuacha katika usajili wao mpya.

 

“Chirwa tumefikia naye muafaka mzuri kwa ajili ya kuichezea Azam baada ya mvutano wa muda mrefu kati yake na uongozi kabla ya kukubali kusaini mkataba mpya.

 

“Mvutano huo ulikuwepo kwenye dau la usajili ambalo yeye alikuwa akihitaji ni kubwa, lakini nashukuru tumefikia muafaka mzuri na kusaini mkataba,”alisema Jaffar. Aidha Azam jana ilimuongeza mkataba wa miaka mawili kiungo mchezeshaji, Salmin Hoza

Stori na Wilbert Moland

Comments are closed.