The House of Favourite Newspapers

IGP SIRRO ASHIRIKI MBIO ZA KM 10 ZA MARATHON

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewaongoza vijana wa rika mbalimbali katika mashindano ya mbio za Dassani Marathon KM 21, KM 10 na KM 05 zilizofanyika jijini Dar es salaam, huku wengine kadhaa wakijinyakulia zawadi kwa kuibuka washindi kwenye mbio hizo.

 

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ambapo IGP Sirro akiwa mgeni rasmi kwenye mashindano hayo pia alishiriki kwenye mbio za KM 10, IGP Sirro, amesema kuwa, suala la vijana kushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya michezo kutasaidia kuwaepusha kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu.

Comments are closed.