The House of Favourite Newspapers

Lugola: Wanaozusha utekaji, na kupotea watu wakamatwe

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,  amelitaka Jeshi la Polisi kuwafikisha mahakamani watu wanaoeneza taarifa za uogo kuhusu kutekwa na kupotea kwa watu, jambo linaloipaka matope serikali.

 

Lugola alisema hivyo alipokuwa akijibu swali la mwananchi Mnyaga Semba, katika mkutano kwenye  Kata ya Kisorya, Mwibara, Bunda, Mkoani Mara, aliyeuliza kuhusu watu kutekwa na hata kupotea, mmoja wao akiwa Azory Gwanda, aliyekuwa mwandishi wa habari.

 

Lugola ambaye yuko jimboni kwake Mwibara akikutana na wapiga kura wake na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, alisisitiza kwamba watu wanaozusha habari hizo kupitia mitandao wachukuliwe hatua mara moja.

Comments are closed.