The House of Favourite Newspapers

Mzee Chillo: Bongo Muvi Kuna Wavamizi, Wapenda Kiki!

Mzee Chillo akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Global TV, Grace Khuni.

MUIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya Bongo Muvi, Mzee Chillo, leo Septemba 26, 2019 amefika katika mjengo wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kufanya mahojiano na Global TV Online na +255 Global Radio.

 

Akifanya mahojiano na kipindi cha Mid Morning Fresh cha +255 Global Radio, Chillo amesema sio watu wote ambao wanatoa filamu wana utaalamu wengine wamevamia huku akisema kuwa anajivunia kufahamika tokea ameanza muvi mtaani mpaka Ikulu na amepata nafasi ya kusafiri nje ya nchi na kujuana na watu mbalimbali.

…mahojiano yakiendelea.

Pia ameponda tabia ya wasanii kuendekeza kiki kabla ya kutoa kazi huku akisema wanatakiwa kutoa kazi iliyo bora ambayo itapendwa na watu.

 

Aidha, amewataka baadhi ya madairekta nchini kuacha tabia ya kuwapa wasichana nafasi za kuigiza kwa kigezo cha urembo wao jambo ambalo linadhorotesha tasnia ya uigizaji.

 

Amesema kuwa watu wengi hasa wanawake wanachukulia uigizaji kama ni sehemu ya kuuza sura hivyo wengi wao wanaingia kwenye fani hata kama hawana wito wa kuigiza.

…akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho.

Pia amewataka waigizaji wakongwe kuwapa ushirikiano waigizaji chipukizi na kwamba wao ndio sababu ya kukuza vipaji vya wanaochipukia.

Hata hivyo, Mzee Chillo ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapatia lakini ameiomba iwaruhusu kufanya baadhi ya vitu kiuhalisia ikiwa ni pamoja na kutumia bastola, vituo vya polisi na vingine ambavyo vitaonesha uhalisia.

 

SABABU ya VIJANA KUJIUA ni HII – MUHIMBILI WATOA TAMKO

Comments are closed.