The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kutaka Kumpindua Rais

Mamlaka za Usalama zimewakamata watu watatu pamoja na vifaa vya milipuko na silaha zingine za kivita wakidaiwa kupanga njama za kuipindua Serikali ya Rais Nana Akufo-Addo.

 

Vikosi vya usalama katika Taifa hilo la Afrika Magharibi vimesema vilikuwa vikifuatilia shughuli za watuhumiwa hao kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuwakamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Watuhumiwa hao bado wanahojiwa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Comments are closed.