The House of Favourite Newspapers

BetPawa Ilivyotangaza Washindi Wa Dream Maker Season 2

0
Meneja wa Masoko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu (kati kati) akiwa katika picha pamoja na baadhi ya washindi wa Dream Maker msimu wa pili. Kulia ni Anania Muba na kushoto ni Herman Mwakatobe.

Dar es Salaam, 6 Desemba 2023 :Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya BetPawa leo imewatangaza na kuwakabidhi zawadi zao washindi wa Dream Maker Season 2 kwenye hafla iliyofanyika jijini ambapo kabla ya yote Meneja Masoko wa BetPawa Tanzania, Borah Ndanyungu alianza kwa risala kama ifuatavyo;

“Naitwa Borah Ndanyungu. Mimi ni Meneja Masoko  wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania.

Napenda kuwashukuru sana wote kwa kuja kushiriki nasi katika siku hii muhimu tunapokwenda kuwatangaza washindi wetu wa awamu ya pili ya kampeni yetu ya Dream Maker.

Wakati tunakwenda kuwatangaza washidi wa awamu hii ya pili, napenda kuwakumbusha kuwa katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa ni mwezi Septemba 2021, BetPawa iliwashika mkono Watanzania wenzetu 13 kutimiza ndoto zao kwa kuwezesha kujenga nyumba mpya, kujenga viwanja vya michezo na kuanzisha biashara mpya hivyo kusaidia kutengeneza fursa mpya za ajira. 

Mabibi na Mabwana;

Kama mnavyojua, lengo kubwa la BetPawa Tanzania ni kuwawezesha Watanzania wenye ndoto zao kwa kufanya ubashiri wa michezo kuwa rafiki na kutoa fursa kwa kila mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 kushinda zaidi na kutimiza ndoto zake.

Mmoja wa washindi wa kampeni ya Dream Maker inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BetPawa Tanzania Bw. Ismail Kahanda akielezea namna ambavyo ndoto yake ambayo inakwenda kutimizwa na BetPawa Tanzania itabadilisha maisha yake na jamii inayomzunguka.

Kampeni ya BetPawa DreamMaker ni ya wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea. Kupitia kampeni hii, Watanzania wanawezeshwa kutimiza ndoto zao ambazo kama isingekuwa msaada wa BetPawa pengine isingekuwa rahisi kuzitimiza.

Leo tutashududia ndoto za Watanzania wengine 20 kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini  zikienda kutimizwa na hivyo kubadilisha maisha yao.

Mabibi na mabwana;

Miradi 20 ambayo leo tunatangaza kuwa imefaulu kupitia kampeni ya Dream maker, imepatikana kutokana na mamia ya mawazo na maandiko ya miradi ambayo yalipokelewa moja kwa moja kupitia basi letu lilikuwa linazunguka katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Basi letu lililokuwa linajulikana kama Dream bus lilizunguka katika mikoa  ya Lindi, Mtwara na Ruvuma na kutoa fursa ya watu kupanda na kuelezea ndoto zao.

Tumepokea maombi pia kwa njia nyingine kama za kimtandao na zisizo za kimtandao kupitia video na taarifa ambazo zilitumwa kwenye mitandao ya kijamii kwa hashtag #betPawaDreamMaker.

Timu ya BetPawa ilipitia kwa umakini wa hali ya juu mawazo yote na kupata 20 ambayo yameonekana kuwa bora zaidi na ambayo tutakwenda kusaidia kutimia.

Mabibi na mabwana;

Naomba mniruhusu nitaje baadhi ya ndoto ambazo tunakwenda kusaidia kuzitimiza katika awamu hii ya pili;

Ndoto au miradi 20 ya ambayo inakwenda kupata msaada kutoka BetPawa Tanzania ni pamoja na kusaidia ujenzi wa vituo vya afya, miradi ya maji, miradi ya masoko, majiko sanifu kwa mazingira pamoja biashara mbali mbali.

  1. Herman Mwakatobe wa Mbeya ana ndoto ya kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza majiko sanifu kwa mazingira ambayo yanatumia oil chafu kama nishati ya kupikia.

Majiko hayo rafiki kwa mazingira anasema yataitwa Pawa Cooking na yatatumika majumbani, kwenye migahawa, mashuleni, vyuoni, viwandani na yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.

Kwa kusaidiwa na BetPawa kutimiza ndoto yake hii, ataweza pia kutengeneza ajira mpya ambazo zitasaidia Watanzania wengine.

  1. Betpawa, DreamMaker inakwenda kumwezesha Anania Muba kutoa huduma bora na salama za kiafya kwenye Kiliniki ya Nangomba kwa kuwa jengo linalotumika kwa sasa ni chakavu na siyo salama.

Kwa kusidia ukarabati wa jengo hilo, BetPawa  inakwenda kubadilisha Maisha ya mamia ya familia zinazotumia kiliniki hiyo kupata huduma za kiafya katika eneo hilo.

  1. BetPawa DreamMaker inakwenda kumsaidia Eric Salema kutimiza ndoto yake ya kusaidia kutatua tatizo sugu la ukosefu wa maji huko Sanya Juu mkoani Kilimanjaro. Ndoto yake ni kuchimba kisima kitakachosaidia upatikanaji wa maji ya uhakika kwa ajili ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo.

Kwa kutekeleza mradi huu, BetPawa itawezesha jamii ya kwenye mradi kulima mboga mboga na kupata maji ya uhakika kwa ajili ya matumizi ya majumbani na mifugo yao hivyo kuboresha maisha yao.

Mabibi na Mabwana; 

Hawa ni baadhi tu ya washindi wetu. Kuna wengine wengi wakiwamo;

  • Ismail Kahanda ambaye ana ndoto ya kuwasidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya michezo kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao.
  • Yusra Ramadhani ambaye anataka kumiliki mgahawa wa chakula kwa ajili ya kusaidia familia yake na kutengeneza ajira kwa Watanzania wengine.
  • Yuda Maongezi ambaye ana ndoto ya kuanzisha biashara yake ya urembo wa kucha baada ya kuwa amefanya kazi kwa muda mrefu kama mwajiriwa.
  • Bernadeta Hilonga mwenye ndoto ya kununua mashine ya kusaga nafaka kawa ajili ya kujipatia kipato kitakachomsaidia kusomesha Watoto wake.

Majina ya washindi wetu wa awamu hii ya pilii yanpatikana katika tovuti yetu pamoja kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Mabibi na Mabwana,

Tunapenda kuwashukuru sana wote walioshiriki katika msimu huu wa pili wa Dream Maker na haswa wale ambao walileta maombi yao lakini hayakufanikiwa.

Napenda kuwaambia kuwa mawazo na ndoto zao bado zina nguvu na hivyo wasikate tamaa na badala yake  waendelee kupambana ili ziweze kutimia.

Sisi kama BetPawa Tanzania tutaendelea kufanya michezo ya kubahatisha kuwa rafiki na kuwawezesha Watanzania wenye zaidi ya umri wa miaka 18 kubashiri kidogo na kupata ushindi mkubwa ambao utasaidia kutimiza ndoto zao”. Ndivyo alivyomaliza kusema meneja huyo.

Leave A Reply