The House of Favourite Newspapers

Waziri Silaa Ataja Changamoto Sekta Ya Ardhi Wakati Akiwasilisha Randama

0
Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeoleo ya Makazi Jerry Silaa

Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeoleo ya Makazi Jerry Silaa amesema Wizara yake bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa rasilimali watu na fedha, ukosefu wa taarifa sahihi za wamiliki wa ardhi pamoja na ucheleweshaji wa malipo ya fidia kwa wananchi.

Waziri Silaa alizitaja changamoto nyingine kuwa ni malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi, migogoro ya ardhi, uvamizi wa ardhi, na kasi ndogo ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi ikilinganishwa na mahitaji ya ardhi iliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Waziri Silaa alizitaja Changamoto izo mapema jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasilia na Utalii wakati alipofika mbele ya Kamati hiyo kuwasilisha utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake fungu 48 na fungu 03 kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha Kiongozi huyo wa Wizara ya Ardhi alibainisha kuwa zipo juhudi za kukabiliana na changamoto hizi pamoja na yinginezo, kwani Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhakikisha viwanja vyote vilivyopimwa vinamilikishwa kwa wahusika, kuongeza kasi ya uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kama suluhisho la migogoro ya matumizi ya ardhi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by WIZARA YA ARDHI (@wizara_ya_ardhi)

Leave A Reply