The House of Favourite Newspapers

Mandela Sekondari Chalinze Watembelea Ofisi za Global

wanafunzi1-1Wanafunzi wa Kidato cha tatu kutoka katika Shule ya Sekondari ya Mandela, Chalinze, Mkoa wa Pwani wakiwa katika meza ya mhariri kiongozi wa magazeti pendwa, Osca Ndauka, wakifafanuliwa jambo kuhusiana na maandalizi ya magazeti

wanafunzi1-2

…Wakiwa katika meza ya Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amrani Kaima, wakipata maelezo.

wanafunzi1-3

Mhariri wa Msadizi wa  Gazeti la Ijumaa,  Andrew Carlos (wa kwanza kulia) akijibu swali kuhusu namna ya wanavyopanga picha katika gazeti.

wanafunzi1-4

Mwandishi wa hadithi wa Global, Nyemo Chilongani (wa pili kushoto) ambaye aliwaongoza ofisini hapo, akiwa kwenye meza ya Mhariri wa Gazeti la Risasi, Erick Evarist.

wanafunzi1-5

Mmoja wa wanafunzi akimuuliza Nyemo Chilongani (kulia), swali linalohusiana na uandishi wa hadithi .

wanafunzi1-6

.. Chilongani akiwaonyesha mambo mbalimbali yaliyomo ndani ya ofisi hiyo.

wanafunzi1-7

Wakiendelea kupatiwa elimu juu ya uandaaji wa magazeti ya Global.

wanafunzi1-8

Wakiondoka ndani ya ofisi za Global.

wanafunzi1-9

Wakiwa katika picha ya pamoja na Nyemo Chilongani nje ya ofisi hizo.

WANAFUNZI wa kidato cha tatu kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandela iliyopo Chalinze, Mkoa Pwani, leo wametembelea katika ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na gazeti la michezo la Champion iliyopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar es Salaam na kujifunza namna magazeti hayo yanavyoandaliwa mpaka kufikia msomaji.

Wakiongozana na kiongozi wao, Stella Clatus, wanafunzi hao waliwaeleza waandishi wa habari ofisini hapo kwamba wamefurahi kukaribishwa ofisini na waliondoka wakiwa wamejifunza na kuelewa mambo yanayofanywa na kampuni hiyo.
“Tumefurahi kufika hapa, hatukuwa tukijua kama tungeondoka na maarifa kama tuliyoyapata leo yanayohusiana na maandalizi ya gazeti hadi kumfikia msomaji. Tumejifunza mengi kiasi kwamba kila mmoja wetu anatamani kuwa mwandishi wa habari,” alisema Stella.

Comments are closed.