The House of Favourite Newspapers

Mzee Mwinyi Aongoza Matembezi ya Skauti Dar

Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza, akizungumza jambo baada ya kuhitimisha matembezi.

RAIS mstaafu ambaye pia ni Mdhamini wa Skauti Tanzania, Mzee  Ali Hassan Mwinyi,  leo ameongoza matembezi ya hisani (Charity Walk) kwa ajili ya kuchangisha fedha  za kufanikisha shughuli za Chama cha Skauti Tanzania  kutoka kwa wadau na marafiki wa skauti kuelekea maadhimisho ya siku ya Skauti Afrika yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 hadi 11 mwaka huu jijini Arusha.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) alipofika katika viwanja vya Bwalo la Polisi, Oyster Bay jijini Dar, wakati alipohitimisha matembezi ya hisani. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako aliyeungana naye.

Matembezi hayo ya hisani yameanzia katika kiwanja cha Skauti kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam na kuishia katika bwalo la Polisi (Police Mess) la Oyster Bay kuanzia saa 12 asubuhi na kufikia tamati majira ya saa nne asubuhi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa matembezi hayo, Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza,  alisema kuwa chama hicho kinatarajiwa kusherehekea Siku ya Skauti Afrika na kuadhimisha miaka 100 tangu Skauti kuingia Tanzania Bara (Tanganyika).  Chama hicho hapa nchini kilianza mwaka 1917 na mwaka huu wa 2017 kinatimiza miaka 100.

Uchangishaji mwingine wa fedha kwa njia ya chakula (Dinner Gala Fund Raising) unategemea kufanyika Februari 24  katika Hoteli ya Serena ya ijini Dar es Salaam.

 

      

Denis Mtima/GPL

Comments are closed.