The House of Favourite Newspapers

Matunda Yanayosaidia Kupunguza Maumivu ya Tumbo la Hedhi-2

WIKI iliyopita nilielezea baadhi ya matunda yanayosaidia kupunguza maumivu ya hedhi. Leo nitaeleza visababishi vya maumivu hayo. Moja ya kisababishi kikubwa kabisa cha hedhi mbovu yenye kuambatana na maumivu makali ya kiuno, kichefuchefu, kutapika nk husababishwa na mwili wako kuwa na kiwango kingi cha Prostaglandini.

Hiki ni kichocheo na  hutolewa kwenda kwenye ukuta wa kizazi kusaidia kushusha ukuta uliotengenezwa na kuandaliwa kwa kutungisha na kuimarisha mimba kumong’onyoa ukuta huo ili ukuta mwingine utengenezwe ili yaanze maandalizi mapya ya mzunguko unao fuata.

Inapotokea kuwa kiwango hiki cha Prostaglandini  kinakuwa kingi kupita kiasi kinasababisha kule kukuza  na kusinyaa kwa misuli ya mfuko wa kizazi kuwa kwa kiwango cha juu  na wenye kuambatana na maumivu makali sana isivyo kawaida.

JIHADHARI NA VYAKULA

Moja ya baadhi ya vitu vinavyo sababisha kiwango cha Prostaglandini kuwa juu kupita kiasi ni ulaji wa vyakula vinavyo sababisha mchakato mwilini mwako na kuvuruga utendaji kazi wa mwili wako na hatimaye kuvuruguka shughuli zingine.

Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ngano, kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi na rangi kama juisi na soda ambavyo ni kemikali za viwandani. Matumizi ya pombe, kahawa, caffeine zote hivyo ni hatari sana kwa afya ya mwanamke wakati wa mzunguko wake wa hedhi.

Jiepushe kuwa na uzito kupita kiasi ndiyo maana asilimia kubwa ya wanawake wenye matatizo haya ya maumivu ya tumbo la hedhi huwa wana dalili zinazoambatana na matatizo mengine ya mfumo wa chakula kama choo kuwa ngumu, Hemmorhoids  (bawasili), tumbo kuuma/kujigawa na kadhalika.

Hivyo basi unatakiwa pia kuhakikisha huna mchakato wowote unaoendelea kwenye mfumo wa chakula ili uweze kutibu tatizo hilo. Hivyo ndivyo baadhi ya visababishi vya msingi vinavyosababisha Proglandini kuwa katika kiwango cha juu sana na kusababisha misuli ya mfuko wa kizazi kukaza kupita kiasi kwa kuambatana na maumivu makali hasa wakati wa hedhi.

Kuna wanawake wengine wanakuwa na matatizo ya kiafya katika mfumo wa uzazi ambayo sasa yanasababisha hedhi mbovu kwa mwanamke. Aina hii ya kisababishi huitwa kisababishi sekondari, jina hili linatokana na jinsi dalili za hedhi mbovu zinavyotokea baada ya mwanamke kuwa na matatizo ya kuwa hedhi mbovu kwa kuwa na sekondari ya ugonjwa katika mfumo wa uzazi. Magonjwa haya yanaweza kuwa kama Endometriosisi .

Huu ni ugonjwa ambao haujulikani kuwa unasababishwa na nini hadi sasa lakini hauwezi kuambukizwa hata kwa kutumia njia ya kujamiana, huu ugonjwa unasababishwa na zile seli za ukuta wa mfuko wa kizazi zinatoka zinaenda kujipandikiza popote nje ya
mfuko wa kizazi na kuwa na sifa ile ile kama zinapokuwa ndani ya mfuko wa kizazi.

Mbali na endometriosisi pia hedhi mbovu kama dalili ya msingi inaweza kusababishwa na vimbe ambazo zinaota ndani ya mfuko wa kizazi, nje ya mfuko wa kizazi na kwenye misuli ya kizazi ambazo huita fibroids.

Wagonjwa wengi yenye fibroids hulalamika kupata hedhi mbovu.Wanawake wengine huchanyama maumivu wanayo pata wakati wa hedhi na maumivu ya maambukizi kwenye mirija ya uzazi yani PID (Pelvic Inflammatory Diseases) hii ni kwa sababu inaweza kuwa ulipata maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanzo halafu maambukizi hayo yakapanda hadi kwenye mirija ya uzazi na hatimaye kusababisha dalili hizo za kiuno kukaza na kuuma sana lakini ukitaka kutofautisha tatizo hilo zingatia kwamba maumivu yanayotokana na PID hayaambatani na siku za hedhi hivyo ndivyo unaweza kutofautisha kiurahisi kabisa. Itaendelea wiki ijayo.

Na Mwandishi Wetu/GPL

Comments are closed.