The House of Favourite Newspapers

Aina 10 Za Wanawake Wanaopendwa Na Wanaume

Image result for couples goals

KARIBU jamvini mdau, ni Jumatatu nyingine tunakutana tena hapa kupeana elimu ya uhusiano wa kimapenzi na maisha kwa jumla. Nimekwishaeleza mara kadhaa kwamba wote tumezaliwa tukiwa safi kabisa. Mambo mengine hujitokeza huko katikati kadiri tunavyokua na malezi tunayoyapata.

Leo kwenye ukurasa huu nitakudadavulia aina kumi (10) za wanawake wenye tabia fulanifulani ambao ndiyo hupendwa zaidi na wanaume hivyo ukiwa mwanamke na ukawa na tabia hizo, basi ujue wewe ni ‘madini’ kwa wanaume;

1: MSIMAMO

Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo.Wanawake wa aina hii pia huwa na uelewa mkubwa wa mambo na uamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

2: USAWA

Aina ya pili inayohitajika katika ulimwengu wa kimapenzi ni  wanawake wanaoheshimu usawa wa kijinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

3: MAPENZI

Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana na wanaume. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

4: MARAFIKI

Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.Image result for couples goals

5: WA WAZI

Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika uamuzi wa msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za kibabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.

6: WANAOJITEGEMEA

Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na wanawake ‘magolikipa’. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

7: WASIO NA PRESHA

Ukisikia wanawake wasio na presha maana yake ni wasiolazimisha vitu vitokee harakaharaka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kubwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.

8: WASAFI

Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni waelewa wa mazingira na si washamba. Hawa ni wale wanaopendeza kwa muonekano.Related image

9: WANAORIDHIKA

Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini kwenda juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

10: WA MOJA

Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi kutoka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana.

 

Comments are closed.