The House of Favourite Newspapers

Utafiti Twaweza: Nusu ya Watanzania Wako Salama

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali.

UTAFITI uliofanywa na taasisi ya Twaweza umeonyesha kuwa usalama kwa nusu ya Watanzania umeimarika katika mwaka mmoja uliopita kwa asilimia 53 ambapo asilimia 37 walisema hali ya usalama imebaki vilevile na asilimia 10 wanasema hali imekuwa mbaya zaidi.

Utafiti huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, katika mkutano na wadau uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar, alipofafanua kuwa matokeo hayo yametokana na utafiti wake uitwao ‘Hapa usalama tu: Usalama, polisi na haki nchini Tanzania’.

Mkutano na wadau ukiendelea.

 

“Muhtasari huu unatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka sauti za wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika kwenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mkononi.

 

Ni matokeo na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,805 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara bila kuhusisha serikali ya Zanzibar yaliyofanyika Aprili mwaka huu,” alisema.

Na Denis Mtima | GPL

YALIYOMO KWENYE RIPOTI YA TWAWEZA

Lissu Aachiwa Huru, Kesi Yake Kuunguruma Agosti 24

Leave A Reply