The House of Favourite Newspapers

Okwi Aandaa Sapraizi Kwa Mbelgiji

Emmanuel Okwi.

MFUNGAJI bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi, ameonekana kutaka kumshangaza kocha wake mpya wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems kufuatia kauli yake ya kuhusu maandalizi ya msimu ujao.

 

Okwi alifanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao 20 akifuatiwa na John Bocco am­baye alifunga mabao 14, na dalili zinaonyesha anataka kuwashanga­za wengi kwa kutetea tuzo hiyo ya ufungaji bora.

 

Hata hivyo, mshambuliaji huyo mwenye uraia wa Uganda, anatara­jia kukutana na upinzani mkubwa katika mbio za ufungaji bora msimu ujao wa Ligi Kuu Bara una­otarajiwa kuanza Agosti 22 kutoka­na na uwepo wa mshambuliaji wa Yanga, Mkongo, Heritier Makambo ambaye kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa ni mchezaji hatari katika kufumania nyavu.

Akizungumza na Championi Iju­maa, Okwi amesema amejiandaa vizuri kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ili kuendana sawa na ush­indani wa ligi kwa kujituma kuliko msimu uliopita.

 

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, nahi­taji kujituma zaidi msimu ujao ili niweze kufanikiwa kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.

 

“Nahitaji kuanza msimu vizuri kwa kuhakikisha nafani­kiwa kufunga zaidi ya msimu uliopita, ligi itakuwa ngumu na ya ushindani, tunajipanga kuwa vizuri,” alisema Okwi.

 

Upande wa pili, Kocha Aussems amekuwa na matu­maini na safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Okwi na kudai kuwa anaamini wakiendelea kwa kasi hiyo msimu ujao watakuwa hatari zaidi.

 

“Kocha amefurahishwa na namna kiwango pamoja na kasi ya kufunga ya Okwi,” kilisema chanzo cha taarifa.

 

Alipotafutwa kocha mwenyewe alisema: “Wachezaji wote wana­fanya kazi nzuri na wanatimiza vile ambavyo nimekuwa nikivitaka. Kwa sasa tunaangalia zaidi juu ya mechi yetu na Ngao ya Jamii na siyo kitu kingine.”

Stori: Khadija Mngwai na Said Ally, CHAMPIONI IJUMAA

Comments are closed.