The House of Favourite Newspapers

Dar Live kumekucha! watoto wajiachia

0

dar live (1)dar live (2)Watoto wakishindana kuogelea.dar live (3)dar live (4)Watoto wa kike na wa kiume wakishindana kukimbia huku wamevaa magunia.dar live (7) dar live (8)dar live (10)Watoto wakiwa katika bembeadar live (4)Watoto wakiendelea kuburudika kwenye bembea hizo.dar live (5)Hizi ni baiskeli ndogo za watoto.dar live (9)Watoto wakionesha mapozi katika moja ya mabembea yaliyopo ukumbini humodar live (1)

Mmoja wa wazazi (kulia) akionekana kuwa karibu kuhakikisha watoto wanapata burudani za kutosha kwenye bembea za chini.

dar live (2)Burudani mwanzo mwisho kwa watoto kubembea.

Waumini wa dini ya Kiislam nchini, leo wanaungana na waumini wenzao duniani kote kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajji.

Katika kusherehekea sikukuu hiyo, Uwanja wa wa wa taifa wa burudani, Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem umeandaa tamasha lililotambulishwa kama ‘Ammerudi Night’. Tamasha litakaloungurumishwa na msanii maarufu nchini wa nyimbo za dansi, Christian Bella ‘King of the Best Melodies’ atakapowasha moto uwanjani hapo huku akizindua wimbo wake mpya wa Amerudi.

Bella atasindikizwa na wasanii wakali kama, Kadja Nito, Msaga Sumu na wengine wengi.

Tamasha hilo la aina yake litaanza saa 1:00 jioni mpaka majogoo kwa kiingilio cha Tsh. 8,000/= kwa wakubwa na Tsh. 2,000/= kwa watoto.

Tayari michezo na burudani za za utangulizi za watoto zimekwishaanza uwanjani hapo kama picha zinavyoonesha.

PICHA NA STORI: DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply