The House of Favourite Newspapers

Samia Suluhu azuru Kongamano la Wanawake Dar

0

 

5 bWakina mama wakionesha tochi zao juu kama ishara ya wanawake kupata nuru ya uwakilishi serikalini kupitia Bi. Samia Suluhu.
1.Mhadhiri Chuo cha Muhimbili, Dr. Ave Maria Semakafu akiwakaribisha wageni waalikwa.
4b2Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
3Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Pipi akiimba wimbo wa Tanzania Tanzania.5Samia Suluhu akitoa hotuba fupi katika kongamano hilo.6Hapa akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye kongamano hilo.7Katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali wa kongamano hilo.

MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu amezuru kongamano la wanawake wa vyuo vikuu na wanataaluma lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar leo hii.

Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu isemayo: WANAWAKE TUMEWEZA, TUPEWE FURSA ZAIDI,” lilihudhuriwa pia na vikundi vya akina mama wajisiariamali, waliompongeza Bi. Samia Suluhu kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza anayewakilisha wanawake na kumkabidhi changamoto lukuki zinazowakabili kinamama nchini kwa ajili ya kuzitatua pindi atakaposhinda nafasi hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa kuwakabili wanawake ni pamoja na uchache wa huduma za afya kulingana na idadi ya akinamama hasa katika suala la uzazi, kuongezewa zaidi kipaumbele katika soko la ajira na kuongezewa nafasi zaidi za uongozi serikalini.

Katika hotuba yake, Bi. Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo naye aliwapongeza kinamama nchini kwa kushiriki kwenye maendeleo ya taifa zima kwa ujumla huku akipongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya awamu ya nne katika kuweka misingi ya kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali kama vile nafasi za  uongozi serikalini, ajira kwa akina mama hasa serikalini na fursa sawa ya elimu hasa kwa wanafunzi wa kike.

Mbali na hayo Bi. Samia aliwahakikishia wakina mama waliohudhuria kongamano hilo kuwa akifanikiwa kupita katika nafasi hiyo atahakikisha anamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma za afya hasa upatikanaji wa madawa na vifaa vya matibabu kwa kufuatilia zoezi zima la utoaji wa dawa kutoka bohari kuu hadi matumizi ya daktari husika kwenye kila kituo cha afya ili kukomesha wezi wa dawa hizo wanaojinufaisha wao binafsi.

Akizungumzia kuhusu sekta ya elimu, Bi. Samia Suluhu aliwahakikishia wanawake hao kuwa ataboresha sekta ya elimu kwa kuunda taasisi maalumu itakayoshughulikia ajira za walimu na maslahi yao ambayo alisema kuwa hayatakuwa yakisimamiwa na halmashauri tena ili kuepuka usumbufu kwa madai ya walimu nchini.

Picha/ Chande Abdallah/GPL

Leave A Reply