The House of Favourite Newspapers

Mambo yazidi kumnyookea Uhuru Sauz

0

NYOTA wa zamani wa Simba, Uhuru Suleiman sasa anakipiga katika Klabu ya Royal Eagles ya Afrika Kusini kwa mkopo akitarajiwa kurejea Jomo Cosmos, lakini Mamelodi Sundowns nayo inamtaka.

Awali Jomo Cosmos ndiyo iliyomsajili baada ya Simba ‘kumkaushia’ lakini alipofika Afrika Kusini, klabu hiyo ya Ligi Kuu Afrika Kusini ikampeleka kwa mkopo Royal Eagles ya Daraja la Kwanza ili aboreshe kiwango chake.

Kwa mujibu wa Uhuru mwenyewe, sasa yupo vizuri na akiwa katika harakati za kurejea Jomo Cosmos, taarifa zimemfikia kuwa Mamelodi wanataka kumsajili.

“Januari mwakani natakiwa kurejea Jomo Cosmos, lakini wakala wangu ameniambia amefuatwa na watu kutoka Mamelodi wakitaka kunisajili bada ya kuvutiwa na uwezo wangu,” alisema Uhuru.

“Nafurahi kuona mambo yanaenda hivi, lakini hatma ya wapi nitacheza itafahamika Januari kwani ni lazima tufikie makubaliano mazuri.”

Leave A Reply