The House of Favourite Newspapers

Bin Kleb: Nimerudi Kurejesha Heshima…

Abdallah Bin Kleb (kushoto).

 

UNAMKUMBUKA yule jamaa aliyewafanyia umafi a Simba kwenye usajili wa mchezaji Mnyarwanda, Mbuyu Twite? Huyu ni Abdallah Bin Kleb na tayari yeye mwenyewe amesema amerejea Yanga na ameshatoa mchango wake.

 

Bin Kleb alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Kamati ya Mashindano ya Yanga ambapo enzi zake alikuwa moto kwenye ishu za usajili ambapo alifanikiwa kuwazidi Simba mara nyingi kwenye kugombea wachezaji.

 

 

Bosi huyo mwenye  jina na heshima kubwa Yanga, hivi karibuni alitangazwa kuwepo kwenye kamati maalum ya uhamasishaji michango ya klabu hiyo kwa ajili ya usajili katika msimu ujao iliyokuwepo chini ya mwenyekiti wake, Anthony Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Sera, Bunge, Kazi, Ajira na walemavu pia ni mbunge wa Dodoma mjini Bin Kleb ameeleza malengo ya kurejea tena katika timu hiyo kikubwa ni kurejesha heshima iliyopotea katika misimu miwili iliyopita ya kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani wa kitaifa na kimataifa.

 

Alisema kuwa, katika kamati hiyo mpya yeye ni mjumbe na tayari ameshachangia klabu hiyo huku akipanga kuendelea kuichangia zaidi ili kufanikisha malengo ya usajili ya Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera.

 

“Nikiwa kama mjumbe wa Kamati Maalumu ya Uhamasishaji wa Kuichangia Yanga, nimerudi tena kama zamani kwenye klabu yangu hii baada ya muda mrefu kukaa pembeni.

 

 

“Mimi tayari nimeshachangia na nitaendelea kuchangia kwa kuwa naamini uimara na umahiri wa Yanga ni kusajili kikosi bora ili msimu ujao tufanye vizuri katika ligi.

 

 

“Niwatake Wanayanga wenzangu kuichangia Yanga kwa kadiri wanavyoweza ili tumsaidie kocha wetu Zahera apate kikosi imara,” alisema Bin Kleb.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.