The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Waziri Mkuu Azungumzia Miaka 55 ya Muungano – Video

VIAJANA wote nchini wameaswa kuulinda na kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliyozaa TANZANIA ikiwa ni pamoja na kuwaenzi viongozi waanzilishi wa muungano huo ambao walishatangulia mbele za haki na walio hai.

 

Akizungumza katika Kongamano la Vijana Juu ya Historia ya Muungano, Baraka Shamte,  ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Zanzibar na mmoja wa waasisi wa muungano huo, Mohammed Shamte Hamad,  amewaasa vijana wasitumie elimu zao kuwabeza waasisi wa muungano huo bali kuyaenzi mema waliyolitendea taifa la Tanzania na watu wake.

Mkurugenzi wa Muungano, Sifuna Joseph, akizungumza jambo.

Baraka amesema muungano ni muhimu katika vizazi na vizazi hususani kutambua maendeleo na fursa mbalimbali za kimaendeleo, kushirikiana na viongozi waliopo madarakani na kujituma katika utendaji ili kuliletea maendeleo taifa lao kwani vijana wana nafasi kubwa ya kulijenga taifa na kuleta maendeleo chanya katika nyanja mbalimbali kwa kutumia vipaji na elimu zao.

Kwa upande wake,  mratibu wa kongamano hilo, Rahma Riadh Kisuo, alisema  hakuna sababu ya msingi ya kuhitaji kuwa na serikali tatu ndani ya nchi moja ama kuuvunja muungano huo, hivyo vijana waache dhana hiyo ya kuudharau na kuubeza muungano kwa maslahi yao au kwa kutumika kisiasa.

“Miaka 50 hakuna Sababu ya kuubeza muungano wala kuendeleza chuki, kufungua kesi mahakamani sababu ya muungano, Zanzibar na Tanzania Bara ni kitu kimoja na anayeukataa muungano ni mbinafsi, wala siyo mwenzetu, anapaswa kukemewa mara moja,” alisema Rahma.

 

Akizungumza, mgeni rasmi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ni Mkurugenzi wa Muungano, Sifuna Joseph, alisema kuwa muungano ni tunu ya taifa na hivyo vijana wanapaswa kuuenzi na kuudumisha na kwamba changamoto ndogondogo zinazojitokeza zisiuvunje, hivyo vijana wawe chachu ya kuudumisha.

KONGAMANO KARIMJEE: MIAKA 55 YA MUUNGANO Wadau Watoa MAONI

Comments are closed.