The House of Favourite Newspapers

Tume ya uchaguzi yasisitiza amani

0

Jaji Lubuva (Kulia) akiwa na baadhi ya maafisa wa tume ya uchaguzi.Jaji Lubuva (kulia) akiwa na baadhi ya maofisa wa tume ya uchaguzi.

Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali wakinoti mambo muhimu kwenye mkutano huo.Baadhi ya waandishi wa  vyombo mbalimbali wakinoti mambo muhimu kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wadau na viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wadau na viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kwenye mkutano huo.

Kaimu IGP, Abdallah Kaniki akiwa kwenye mkutano huo.Kaimu IGP, Abdallah Kaniki akiwa kwenye mkutano huo.

Prof.Safari akiwa na John Mnyika.Prof. Safari (kushoto) akiwa na John Mnyika.

Na Haruni Sanchawa / GPL

Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damiani Lubuva leo ametoa wito kwa vyama vya siasa kwamba siku ya uchaguzi mkuu baada ya mpigakura kutimiza haki yake aondoke eneo la kituo cha kupigia kura laa sivyo sheria itachukua mkondo wake.

Kiongozi huyo aliyasema hayo alipokuwa katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa  katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa, tume inaongozwa kwa sheria na kila agizo linalotolewa ni kwa mujibu wa sheria hivyo ni vyema viongozi hao wakatii na kuhakikisha wanawapa taarifa wafuasi wao kwamba wakishapiga kura warudi makwao.

Aliongeza kuwa ile dhana ya kwamba baada ya kupiga kura wanachama wabaki kulinda kura ni kinyume na sheria kwani wenye jukumu la kufanya hivyo ni vyombo vya dola.

Naye Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Abdallah Kaniki amesisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga vya kutosha kuhakikisha siku ya kupiga  kura  zoezi linafanyika kwa amani na umakini wa hali ya juu.

Kaniki alisema kwamba kazi ya usalama viachiwe vyombo vya ulinzi na usalama na si mtu binafsi au kikundi flani.

Akasisitiza kuwa atakayekwenda kinyume na maagizo ya tume hatua kali zitachukuliwa na hakuna suala la lelemama kwani kinachotakiwa ni haki pamoja na amani.

Leave A Reply