The House of Favourite Newspapers

Deo Filikunjombe apata ajali

0

chopa
Deo Filikunjombe akiwa kwenye helkopta anayodaiwa kupata nayo ajali.

MBUNGE wa Jimbo la Ludewa, Mhe. Deo Filikunjombe, Kapteni William Silaa na abiria wengine waliokuwa kwenye helkopta 5Y-DKK jana walipata ajali baada ya helkopta hiyo kuanguka kwenye msitu wa Selous.

Deo-Filikunjombe

Deo Filikunjombe.

Kwa mujibu wa taarifa za awali ni kwamba helkopta hiyo ilipata hitilafu katika injini wakati ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Ludewa.

chopa 3

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meya wa Wilaya ya Ilala, Jerry Silaa ameandika hivi:
“Baba yangu Capt. William Silaa akiwa na Mhe. Deo Filikunjombe na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka kwenye msitu wa Selous.

chopa 2

Hakuna mawasiliano ya simu. Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii.

Nawaomba wote kuwa watulivu kwani jambo hili linahitaji umakini wa hali ya juu na ushirikiano wa taasisi nyingi za wizara tofauti.
Tuwaombee wote Mungu awanusuru.”

Silaa

Naye Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia akaunti yake ya Twitter ameelezea kuwa kwa taarifa za awali, Mhe. Filikunjombe na wenzake wote wapo salama na jeshi la polisi linaendelea na juhudi za uokoaji.

zitto

Leave A Reply