The House of Favourite Newspapers

JK: Soka letu linahitaji ‘tingatinga’

0

kikweteRais wa Tanzania anayemaliza muda wake, Dk. Jakaya Kikwete.

RAIS wa Tanzania anayemaliza muda wake, Dk. Jakaya Kikwete ni kama amewaachia wosia wanasoka kwa kusema kuwa kwa kiwango cha soka letu kilivyo sasa, kwa vyovyote vile anahitajika mtu wa kazi ‘tingatinga’ ili kulifisha mbali zaidi.

JK alisema hayo jana kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Viwanja vya Jangwani ambapo alisema kwa ‘levo’ ya soka letu lilipofikia hasa timu ya taifa, Taifa Stars, inayopambana kucheza Kombe la Afrika na lile la Dunia.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa, alisema mtu pekee mwenye uwezo wa kuiwezesha Taifa Stars kufika hatua hiyo ni Dk. John Magufuli ambaye ni mgombea wa urais kupitia chama hicho anayeaminika kwa kupiga kazi.

“Nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuinua michezo nchini, lakini tulipofikia michezo yetu inahitaji mtu tingatinga, mtu ambaye atatufikisha kucheza Kombe la Afrika na Kombe la Dunia,” alisema JK.

Ikumbukwe kuwa katika miaka 10 ya utawala wake, JK amekuwa msaada mkubwa kwa kuwalipa mishahara makocha wa timu ya taifa.

Leave A Reply