The House of Favourite Newspapers

Dar Musica yazinduliwa kwa kishindo

2

Dar Musica (1)Prezidaa wa Dar Musica, Jado Field Force akionesha ubora wake kazini.

Dar Musica (2)Vimwana wa Dar Musica katika pozi baada ya kushuka jukwaani.

Dar Musica (3)Mashabiki wakijimwaya.

Dar Musica (4)Wanenguaji wakifanya manjonjo.

Dar Musica (5)Shabiki huyu baada ya kukunwa alimpandia jukwaani Prezidaa Jado na kukatika nae.

Dar Musica (6)Safu ya waimbaji wa Dar Musica katika ubora wake.

Dar Musica (7)Jado akiwajibika na wanamuziki wake katika kutoa burudani.

BENDI mpya ya Dar Musica chini ya Prezidaa wa zamani wa Mashujaa Musica, Jado Field Force, akishirikiana na wakongwe wenzake, Imma Chocolate, Dullah Ngoma, Ziggy Stone na chipukizi kadhaa usiku wa kuamkia leo ilizinduliwa kwenye Ukumbi wa Highway Night Park, Ukonga Jijini Dar.

Katika uzinduzi huo bendi hiyo ilionesha umahiri mkubwa wa kukopi nyimbo mbalimbali zilizowahi kuwika ulimwenguni pamoja na kupiga vibao vyake viwili inavyotamba navyo ambavyo ni ‘Bongo michongo’ na ‘Chozi la masikini’.

Ikirindimisha burudani ukumbini hapo, bendi hiyo ilionesha umahiri mkubwa wa kupiga sebene zilizowachagiza mashabiki waliokuwa wakivamia stejini kila mzuka ulipowapanda.

Akizungumza na mtandao huu, Jado alisema amejiandaa kuuteka muziki wa dansi hapa nchini na kunyakua tuzo mbalimbali.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

2 Comments
  1. Kirumbi says

    Hongera sana JADO FILED FORCE. Hii ndio kitu tunataka, ila kaza buti ili usishushe bendera mapema

  2. Kirumbi says

    Hongera sana JADO FIELD FORCE. Hii ndio kitu tunataka, ila kaza buti ili usishushe bendera mapema

Leave A Reply