The House of Favourite Newspapers

Watu 7 wauawa kinyama Burundi

0

Mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa baada ya kutokea kwa mauaji hayo.

Watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu saba usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura Watu hao waliokuwa katika kilabu cha burudani mjini Bujumbura waliamrishwa walale chini kabla ya kufyatuliwa risasi na kuuawa papo hapo.

Wakazi wa Bujumbura wakiyakimbia makazi yao kutokana na machafuko hayo.

Meya wa mji huo ametaja kisa hicho kama mauwaji ya kinyama.Waliwaua watu 7 na kuwajeruhi wengine wawili alisema Freddy Mbonimpa meya wa mji huo. Awali wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu ya Mauaji hayo.

Awali Serikali ilikuwa imewapa watu fursa ya kusalimisha silaha walizo nazo laa sivyo polisi wachukue hatua kali dhidi yao ya kuwapokonya.

Hapo jana wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu ya makabiliano na vyombo vya serikali. Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, aliwaona watu wamebeba magodoro na kadhalika katika mabarabara, wakihamia kwa jamaa na marafiki zao.

Katika juma lilopita pekee , watu 20 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu. Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje. Katika wimbi la machafuko ya kisiasa nchini humo, tangu mwezi Aprili, pale rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.

(Chanzo: BBC)

Leave A Reply