The House of Favourite Newspapers

TCAA Yazuia Mashirika 3 ya Ndege Kenya Kufanya Safari TZ

0

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezizuia kampuni tatu za ndege kutoka Kenya, ambazo ni Air Kenya Express, Fly 540 na Safarilink Aviation kufanya safari zake nchini kutokana na mvutano unaoendelea baina ya nchi hizo hasa sakata la Covid-19.

 

Hii imekuja ikiwa ni wiki chache baada ya Kenya kutangaza nchi 130 ambazo wananchi wake wanaruhusiwa kuingia nchini humo bila masharti ya kuwekwa karantini ya siku 14 wakati Watanzania wanaoingia Kenya wakitakiwa kuwekwa karantini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa TCCA, Johari Hamza, mashirika hayo yaliyozuiwa, ndege zake hufanya safari zake kila siku kati ya Kilimanjaro na Zanzibar.

 

Agosti 1, 2020, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilifuta kibali kilichokuwa kikiruhusu ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania, uamuzi huo ulikuja baada ya Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake waliruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 1. Ndege za Kenya zilisitishwa kutua katika uwanja wa ndege wa JNIA – Dar es Salaam, KIA – Kilimanjaro, wala AAKIA – Zanzibar.

 

 

“Tumezifungia ndege za Kenya kwa sababu Tanzania bado inawekewa vikwazo vizito kule Kenya, kwa hiyo na sisi tumerithishwa guility (hatia) bila sababu.

 

“Ili kumaliza hili suala la kuruhusu ndege kati yetu na Kenya, ni mazungumzo tu na wao (Kenya) watakapokuwa tayari na sisi tutakuwa tayari kwa mazungumzo maana sisi hatuna tatizo la kuzungumza na kuweka mambo sawa,” – Hamza Johari, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Anga nchini (TCAA).

TCAA haikutoa sababu zozote za vizuizi hivyo, mbali ya kuyajulisha mashirika hayo kwamba taarifa hiyo inaondoa vibali vilivyoyaruhusu kuingia  Tanzania.

 

 

Leave A Reply