The House of Favourite Newspapers

Kuna viumbe wengine nje ya dunia tunayoishi?

0

planets_imageILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilieleza namna ambavyo viumbe wanaosadikiwa kuishi angani wa Aliens walivyohusishwa na ule upotevu wa ndege kubwa aina ya Boeng 777 ya Malaysia, Machi, mwaka jana ikiwa na watu 239. SASA ENDELEA…

Katika tukio hilo, wengine walidai kwamba ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuruka umbali mrefu wa saa saba kama ilivyoelezwa kisha kutoka nje ya nguvu ya mvutano (gravitational force) hivyo kushindwa kurudi duniani.

Katika ishu hiyo iliyozua hofu duniani, kuna baadhi ya watu walisema huenda ndege hiyo ilivutwa na Mkondo wa Pembetatu ‘Bermuda Triangle’ uliopo Kusini mwa Bahari ya Atlantiki (nilishaeleza huko nyuma) ambapo eneo hilo limekuwa likihusishwa na upotevu wa ndege za kijeshi na meli kubwa za mizigo.

Baadhi ya wataalam wa sayansi wa kimataifa wanaiita sehemu hiyo makao makuu ya shetani kwa kuwa wenyewe hawajawahi kufika licha ya kwamba ni hapahapa duniani na wameweza kufika mwezini.

Kuhusu Aliens, wanasayansi wanakubali kuwa huenda ndiyo waliohusika na upotevu wa vitu na watu duniani.

Baadhi ya wataalam wa anga wanasema viumbe hao wenye shepu mbaya huenda wakahusika na kuitwaa ndege hiyo ya Malaysia na kuipeleka wanakojua wao.

Wataalam wa anga wanasema kwamba ulimwengu tunamoishi ni mkubwa sana hivyo lolote lawezekana. Wanasema ni mkubwa kupindukia na kila tunachoweza kuona kwa macho au kwa teknolojia ya juu kabisa, ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu huu.

Kwa mujibu wa wanahisabati, tunachoweza kukiona ni kipenyo chenye urefu wa miaka bilioni 46 ya kusafiri kwa mwanga. Hii inaweza kuelezewa hivi; kama kuna nyota imelipuka leo katika kona moja ya mwisho ya upande mmoja wa ulimwengu huu, baada ya miaka bilioni 46 kiumbe aliyeko katika sayari upande wa pili wa ulimwengu ataona mlipuko huo. (hii ni iwapo mwanga huo utaweza kufika).

Ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana angani zinazofanana na jua tunaloliona katika maeneo mengine ya mbali sana katika ulimwenguni huu.
Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na jua tunaloliona ni kati ya asilimia tano hadi ishirini ya nyota zote katika ulimwengu tunayoweza kuiona.

Hii ina maana kuwa pale tusipoona basi kuna uwezekano anga linaendelea mbali zaidi au kuna vitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona tu.

Inaelezwa kwamba uwezekano wa kuwepo sayari zenye maisha ni mkubwa ingawa maisha yanaweza yasiwe haya tunayoyajua sisi.

Utafiti wa kisayansi uliyofanywa na PNAS (Proceedings of the National Academy of Sciences) unapendekeza kwamba kuna angalau asilimia moja ya sayari zinazofanana sana na dunia yetu katika hizi nyota zinazofanana na jua tunaloliona.

Hapa ndipo inakuja dhana ya kuwa kuna viumbe wengine nje ya sayari yetu ya dunia lakini kuhusu uwepo wa binadamu kwenye sayari hiyo tofauti na duniani hakuna uhakika ingawa lolote linawezekana.

Inaelezwa kwamba mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe hao katika sayari nyingine. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo.

Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Lakini wanasayansi wamekuwa wakisema kuwa tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia mia na binadamu.

Inaaminika kwamba jinsi kila kitu kinavyoonekana leo ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadiri muda unavyoenda.
Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na teknolojia kubwa sana zaidi yetu, hili ni wazi na lina sababu zake.

Kama kuna kiumbe kikifika katika sayari yetu basi hii ina maana teknolojia inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo mmoja.

Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa teknolojia ya usafiri tuliyonayo sasa. Mwendo wake ni miaka elfu sabini njiani kutoka hapa na kufikia nyota jirani kwa spidi kali kabisa.

Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply