The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mkurugenzi wa Radio ORS Afariki Dunia

0

MKURUGENZI  na mwanzilishi wa taasisi kadhaa nchini ikiwepo kituo cha Radio ORS ya Terati wilaya ya Simanjiro, Martin Ole Sanago amefariki duniani leo asubuhi katika hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ya Seliani Ngaramtoni, mkoani Arusha.

 

 

Akizungumza Gidion Sanago,mdogo wa Martin, amesema kaka yake amefariki baada ya kuumwa kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Selian iliyopo Ngaramtoni, Arusha.

 

 

 

Amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na taarifa rasmi itatolewa kwani msiba huo, umeacha pengo kubwa katika jamii hasa kutokana na uwekezaji wake maeneo mengi nchini.

 

 

Akizungumzia kifo cha Martin,Mkurugenzi wa mtandao wa mashirika ya wafugaji, wawindaji na waokota matunda nchini,(PINGOS), Edward Porokwa amesema Martin atakumbukwa mchango mkubwa katika jamii, ikiwemo kuanzisha viwanda vya maziwa katika maeneo ya Arusha, Simanjiro, Same na maeneo mengine nchini na kuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Ilaramatak.

 

 

Amesema Martin pia ni mmoja wa waanzilishi wa Kituo cha sheria za haki za binaadamu (LHRC), Mwanzilishi shirika la PINGOs Forums, Mwanzilishi wa Shirika la Enyuata Maa, pia alifanya kazi katika kufanikisha sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na kuanzishwa shirika la haki ardhi.

Leave A Reply