The House of Favourite Newspapers

Kaze, Vladimir Kurejea Burundi Kesho

0

INAELEZWA aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze na kocha wa makipa wa timu hiyo, Vladimir Niyonkuru wanatarajia kuondoka nchini wikiendi hii kurejea kwao Burundi baada ya kutimuliwa ndani ya timu hiyo.

 

Kaze na Niyonkuru wote ni raia wa Burundi ambao wote ni raia wa Burundi wametimuliwa kwenye timu hiyo kufuatia mwenendo wa matokeo mabaya Yanga katika mechi za timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa, limezipata zinasema kuwa makocha hao tayari wameshamalizana na uongozi wa timu hiyo juzi Jumatano na wanatarajiwa kuondoka wakati wowote nchini.

“Kocha Kaze na kocha wa makipa Vladimir wote wameshamalizana na Yanga, (leo) juzi Jumatano na wenyewe wanatarajia kuondoka katika hizi siku mbili kwa kuwa bado wanafuatilia tiketi za ndege,” alisema mtoa taarifa.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta aliyekuwa kocha wa makipa, Vladmir Niyonkuru ambaye amekiri kuwa yupo katika mipango ya kuondoka nchini kutoka sasa baada ya kumalizana na uongozi wa timu hiyo.

 

“Nadhani kati ya Jumamosi au Jumapili naweza kurejea nyumbani ila kwa sasa nafuatilia ndege pamoja na kuweka sawa baadhi ya mambo yangu, nitaondoka na kocha Kaze pamoja,” alisema Niyonkuru.

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply