The House of Favourite Newspapers

Zahera Aanza Kazi Simba Kimyakimya

0

TAARIFA za uhakika zinabainisha kwamba, aliyekuwa Kocha wa Yanga raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera, tayari ameanza kazi ndani ya Klabu ya Simba akiwa Mkuu wa Idara ya Kusaka Vipaji ambapo jana Jumatatu alitarajiwa kutangazwa rasmi.

 

Hii ni mara ya pili kwa Zahera kutajwa ndani ya Simba ambapo awali ilielezwa atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi muda mchache baada ya Sven Vandenbroeck kuondoka.

 

Mmoja wa watu wa ndani kutoka Simba, ameliambia Spoti Xtra kwamba, Zahera ameanza kazi kwa muda wa miezi mitatu sasa huku uwepo wake huo ukifanywa kwa siri kubwa sana.

“Ni kweli hilo suala la Zahera kuwa mkuu wa masuala ya kusaka vipaji ingawa bado limekuwa siri kwa kuwa uongozi wenyewe hautaki presha kutoka kwa mashabiki kutokana na hali ilivyo ndani ya timu.

 

“Ninachojua kwamba atakuwa anashughulikia mambo ya uvumbuzi wa vipaji vya wachezaji, kushauri katika mambo ya usajili, kufanya tathmini ya kikosi kimkakati pamoja na kibiashara na kimasoko.

 

Tayari ameanza jukumu hilo kwa muda wa miezi mitatu sasa,” alisema mtoa taarifa huyo.Spoti Xtra lilimtafuta Zahera kwa njia ya simu, ili kutolea ufafanuzi suala hilo, ambapo iliita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

 

Kwa upande wa viongozi wa Simba, walipotafutwa, wote hawakupatikana akiwemo Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kaimu Katibu Mkuu, DK Arnorld Kashembe.Zahera anakumbukwa zaidi ndani ya kikosi cha Yanga alichokiongoza kwa misimu miwili, 2017/18 na 2018/19 ambapo aliachana na timu hiyo Desemba 2018.Wakati akiwa Yanga, pia alikuwa Kocha Msaidizi wa DR Congo, kikosi kilichocheza AFCON 2019.

 

Kwa sasa Simba ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, benchi lao la ufundi linaongozwa na watu kutoka mataifa manne. Gomes (Ufaransa), Kocha Msaidizi, Seleman Matola (Tanzania), Kocha wa Makipa, Milton Nienov (Brazil), Kocha wa Viungo, Adel Zrane (Tunisia), Dokta, Yasin Gembe (Tanzania), Meneja, Patrick Rweyemam (Tanzania) na Mtunza Vifaa, Hamis Mtambo (Tanzania)

STORI: IBRAHIM MUSSA NA WILBERT MOLANDI

Leave A Reply