The House of Favourite Newspapers

Jeshi Lavunja Serikali ya Chad, Mtoto wa Deby Kuwa Rais wa Mpito

Kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby kilichotangazwa jana Aprili 20, 2021 imeelezwa Jeshi litaongoza Nchi kwa kipindi cha miezi 18, na Baraza litaongozwa na Mtoto wa Rais, Mahamat Kaka, ambaye pia anafahamika kama Mahamat Idriss Deby.

 

 

Mbali na kutangaza kifo cha Rais Deby aliyekuwepo madarakani tangu 1990, Jeshi pia limetangaza kuvunjwa kwa Serikali na Bunge. Mipaka ya anga na ardhi imefungwa, vilevile zuio la kutotoka nje kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 alfajiri limetangazwa.

 

 

Chad itaomboleza kwa kipindi cha siku 14 kufuatia kifo cha Deby ambacho kwa mujibu wa Jeshi, kimetokana na majeraha aliyopata alipotembelea Wanajeshi waliokuwa mstari wa mbele kupambana na kundi la waasi.

 

 

Taarifa ya ghafla ya kifo chake pamoja na maswali kuhusu mazingira halisi ya jinsi kilivyotokea kinaibua simtofahamu Nchini humo. Jeshi limehakikisha kuwa taratibu zote uhakikisha Usalama na Amani zimechukuliwa.

 

Comments are closed.