The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Burkina Faso Lamshikilia Rais

0

Ripoti kutoka nchini Burkina Faso zinaeeleza kuwa wanajeshi walioasi wanamshikilia Rais wa nchi hiyo Roch Kaboré.

Wanajeshi hao wametaka kufutwa kazi kwa wakuu wa kijeshi na kuongezewa rasilimali zaidi ili kupambana na wanamgambo wa Kiislamu.

Machafuko hayo yanajiri wiki moja baada ya wanajeshi 11 kukamatwa kwa madai ya kupanga mapinduzi.
Burkina Faso imekumbwa na misukosuko ya ukosefu wa udhabiti tangu ilipopata uhuru mwaka 1960, ikijumuisha mapinduzi kadhaa.

Jina la nchi hiyo, linalomaanisha “ardhi ya watu waaminifu” lilichaguliwa na afisa mwanamapinduzi Thomas Sankara ambaye alichukua mamlaka mwaka wa 1983. Alipinduliwa na kuuawa mwaka wa 1987.

Tangu mwaka wa 2015, nchi hiyo imekuwa ikipambana na waasi wa Kiislamu waliosambaa kutoka nchi jirani ya Mali. Hii imechochea hasira katika jeshi na kuharibu tasnia muhimu ya utalii nchini humo.

Leave A Reply