The House of Favourite Newspapers

Wafanyakazi wa Kike Walazimishwa Kusalia Majumbani Mwao, Afghanistan

0
Wafanyakazi wa kike nchini Afghanistan waandamana kupinga mfumo dume nchini humo

NI mwaka sasa kuanzia kundi kubwa la Wapashtun, wenye imani kali ya Kiislamu (Taliban) kuchukua nchi ya Afghanistan.

 

Wakati uchumi wa Afghanistan ukiwa umedorora sana kutokana na vikwazo vya Magharibi dhidi ya Taliban, Taliban imewazuia wanawake wanaofanya kazi serikalini kuingia katika maeneo yao ya kazi na kuwalipa mishahara midogo sana ili kusalia majumbani.

Kabla ya Taliban kuchukua uatwala nchini Afghanistan wanawake walikuwa 22% katika ajira

Wakati huo huo, katika sekta binafsi pia, mashirika kadhaa yamepunguza idadi ya wafanyakazi wa kike kwa sababu ya uhaba wa fedha, kulazimishwa na Taliban au kama hatua ya tahadhari ili kujiepusha na Taliban.

 

Kabla ya Taliban kuchukua nchi, wanawake walikuwa asilimia 22 ya wafanyakazi wa Afghanistan ambayo bado ni asilimia ndogo kutokana na mfumo dume nchini humo, katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ilionesha kupungua kwa idadi  ya ajira kwa wanawake kwa 16% nchini Afghanistan katika miezi michache baada ya Taliban kuchukua madaraka huku kwa upande wa wanaume ajira zilishuka kwa asilimia 6.

Ajira kwa wanawake nchini Afghanistan imepungua kwa 16%

Hata hivyo, wanawake nchini Taliban wamekusanyika na kutaka kufanya mazungumzo ya amani na Taliban ili kurudi maofisini mwao.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply