The House of Favourite Newspapers

Marekani Yaionya Urusi Juu ya Utumiaji wa Silaha za Nyuklia Nchini Ukraine

0
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan

NCHI ya Marekani imetoa onyo kali kwa nchi ya Urusi kuwa itajibu mapigo mara moja endapo kama nchi hiyo itatumia silaha za nyuklia katika ardhi ya Ukraine.

 

Hiyo imeibuka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi kubainisha kuwa Mikoa iliyojitenga baada ya kupiga kura za maoni za kujiunga na Urusi itapewa ulinzi wa kutosha dhidi ya wavamizi.

 

Kuchukuliwa kwa maeneo manne ya Luhansk, Donetsk, Kherson na Zaporizhia kuwa ndani ya Urusi kumeamsha hisia nyingine za kuwepo na uhasama wa moja kwa moja kati ya Urusi na majeshi ya NATO lakini pia na Mataifa ya Magharibi.

Rais Putin amesema Urusi itatumia kila njia kulinda mipaka yake

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan amesema Marekani itajibu mara moja hatua yoyote ile itakayochukuliwa na Urusi juu ya matumizi ya silaha za nyuklia na tayari imeshaijulisha Moscow ni kiasi gani cha madhara itakipata endapo kama itajaribu kutumia silaha za nyuklia katika ardhi ya Ukraine.

 

“Kama Urusi itavuka mpaka, kutakuwa na madhara makubwa sana yatakayo ikumba nchi hiyo kwani Marekani itajibu mapigo mara moja.” alisema Sullivan wakati akiongea na kituo cha Televisheni cha NBC.

Majeshi ya Ukraine yakiendelea na harakati za kulinda mipaka ya nchi yake dhidi ya majeshi ya Urusi

Aidha onyo hilo la marekani limechagizwa pia na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Urusi Vladimir Putin aliyesema kuwa nchi yake ipo tayari kutumia kila aina ya silaha na zana za kivita ili kulinda mipaka na nchi kwa ujumla.

 

Leave A Reply