The House of Favourite Newspapers

UWT Sengerema Yapata Mwenyekiti Mpya

0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wawanawake (UWT) Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Jeni Msoga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo wakifurahia ushindi huo.
...Eric Shigongo (kushoto) akiwapongeza akina mama kwa kumaliza uchaguzi salama.

 

Aliyekuwa mwenyekiti wa (UWT) wilaya ya Sengerema Costansia Faida ambaye alikuwa anatetea nafasi yake amepoteza nafasi hiyo baada ya kushindwa na mpinzani wake Jeni Msoga aliyepata kura 381 huku aliyekuwa akitetea nafasi yake Costansia Faida amepata kura 166 na Rosemary Linda amepata kura kura 3 huku kura 2 zikiharibika.

 

Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa ni kura 552 kati ya hizo kura 2 ziliharibika. Kutokana matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi, Sarah Paul amemtangza Jeni Msoga kuwa mwenyekiti wa umoja wa wawanawake (UWT) wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Amewataka walioshiriki uchaguzi huo kushirikiana na mshindi ili kupeleka mbele jumuiya hiyo.

Kwa upande wake mshindi wa nafasi hiyo ya uenyekiti, Jeni Msoga amewashukuru waliompatia kura na kuahidi kushirikiana na wote na kuondoa makundi ili jumuiya hiyo iweze kusonge mbele kimaendeleo.

 

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema Mhusini Zikatimu amewasihi akina mama kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kumaliza makudi kuendela kukijenga chama hicho katika kuelezea yale yote mazuri yanayoendelea kufanyika katika jamii.

Leave A Reply