The House of Favourite Newspapers

Ronaldo: Simheshimu Ten Haag kwa Sababu Yeye Mwenyewe Haniheshimu

0
Cristiano Ronaldo amefanya mahojiano na mwandishi wa habari Piers Morgan

NYOTA wa Manchester United na moja kati ya wachezaji bora duniani wa muda wote Cristiano Ronaldo ameibuka na kuzua mjadala katika mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya Habari baada ya kusema bayana kuwa hawezi kumheshimu kocha wake Erik Ten Haag kutokana nay eye mwenyewe kutomheshimu nyota huyo.

 

Katika mahojiano ambayo amefanya na mwandishi wa Habari Piers Morgan, Ronaldo amebainisha kuwa sababu ya kutoelewana na kocha huyo ni kutokana na kuhisi kusalitiwa ndani ya klabu hiyo kutokana na baadhi ya watu wakubvwa ndani ya klabu ya Manchester United ambao kwa namna moja au nyingine hawataki na walikuwa hawataki yeye kuwepo ndani ya klabu hiyo.

 

Ronaldo amemtaja kocha wake Erik Ten Haag kuwa hataki yeye kuwepo ndani ya klabu hiyo na baadhi ya viongozi wengine kama wawili au watatu na hiyo ni tangu mwaka jana aliporejea kwa mara ya pili ndani ya klabu hiyo.

Cristiano Ronaldo akipokea maelekezo kutoka kwa kocha wa Manchester United Erik Ten Haag

Aidha nyota huyo ameelezea kuwa klabu hiyo imekuwa haina mwendelezo mzuri na haifanikiwi tangu alivyoondoka kocha Sir Alex Ferguson, huku akibainisha kuwa kurejea kwake ndani ya Old Trafford aliusikiliza moyo wake tu pamoja na ushauri kutoka kwa Sir Alex Ferguson ambaye alimuambia kuwa haiwezekani yeye kujiunga na Manchester City.

Ronaldo anatarajiwa kuingoza Timu ya Taifa ya Ureno katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar 2022

Ikumbukwe kuwa wakati Cristiano Ronaldo anaondoka Juventus alikuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester City ingawa mpango huo haukuwezekana na hatimaye akajiunga na mashetani wekundu Manchester United.

 

Kumekuwa na Habari za nyota huyo kutoelewana na kocha wake mkuu Erik Ten Haag kiasi kwamba amekuwa akipata nafasi mara chache sana ya kujumuishwa na kikosi cha kwanza cha mashetani wekundu.

Leave A Reply