The House of Favourite Newspapers

Fainali Carabao Cup… ‘Rashford Bora Kuliko Erling Haaland Kuchukua Mchezaji Bora’

0
Marcus Rashford na Erling Haaland (kulia).

MKONGWE wa Liverpool, Jamie Carragher, amefunguka kwamba, Marcus Rashford anastahili Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Premier League 2022-23 mbele ya Erling Haaland.

Haaland ametua Manchester City msimu huu na hadi sasa amefunga mabao 26 na asisti nne katika mechi 23 za michuano yote.

Carragher amesema, Rashford ambaye anaitumikia Manchester City, ndiye anastahili tuzo hiyo kwani amekuwa bora msimu huu.

Rashford amekuwa moto tangu kumalizika kwa Kombe la Dunia 2022 ambapo hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 10 katika mechi 10.

Imeelezwa kuwa, kura zinatarajiwa kuanza kupigwa hivi karibuni ndani ya Premier League, hivyo Carragher anaamini Rashford anastahili kuwa mshindi.

“Haaland alianza vizuri mara baada ya kutua Manchester City na amesalia kuwa katika nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa Premier League.

“Lakini Rashford chini ya Erik ten Hag ameibeba Manchester United na kuipeleka katika levo nyingine. Amebadilika sana msimu huu na huwezi kumfananisha na Haaland.

“Haaland kwenye kufunga ameisaidia timu yake kwa namna fulani, lakini Man City kuna kitu kama kimepungua kwa upande wao. Pale Haaland anaposhindwa kufunga Man City inakuwa katika wakati mgumu na mchezaji bora siku zote anatakiwa kuipambania timu yake katika nyakati ngumu kupata ushindi.

“Hata hivyo kwa Rashford anakuwa bora akifunga na kuipa ushindi timu yake akiwa tishio katika mechi 24 alizocheza,” alisema Carragher.

DIAMOND PLATNUMZ AMNUNULIA MAMA DANGOTE SAA ya BEI MBAYA, AMJIBU ZUCHU…

Leave A Reply