The House of Favourite Newspapers

Breaking: Rais Samia Afanya Uteuzi Mpya Mawaziri, Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa

0

Rais Samia Suluhu Hassani amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa mitatu ya Shinyanga, Tanga na Songwe.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 26, 2023 na Kurugenzi ya mawasiliano Rais Ikulu imeeleza kuwa wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa ni Christina Mndeme ambae anakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael nae ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe,

Hata hivyo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amehamishiwa Mkoa wa Tanga, huku aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Omary Mgumba uteuzi wake ukitenguliwa.

Katika uteuzi huyo Christina Mndeme anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ambae alichaguliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

 

Leave A Reply