The House of Favourite Newspapers

Wanachama wa LAPF Kufaidika na Mkopo wa Anza Maisha

0

NSEKELA LAPFKaimu afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja Wadogo (Chief Retail Banking) – Abdulmajid Nsekela akitoa wasilisho juu ya huduma mbali mbali zitolewazo na NMB kwa wateja kutoka kwenye taasisi katika mkutano mkuu wa 8 wa Mwaka wa wanachama wa mfuko wa LAPF jijini Arusha.

Benki ya NMB imetambulisha mkopo mpya kwaajili ya wanachama wapya wa mfuko wa pensheni wa LAPF, mkopo huu unaitwa Anza Maisha.

Wanachama wapya wa LAPF watapata fursa ya mkopo wa kuanzia maisha kipindi ambacho bado hawana sifa za kupata mikopo ya maendeleo kupitia benki mbalimbali angalau kwa miezi sita ya mwanzo toka kuwa wanachama wa mfuko wa LAPF.

Mkopo huo utatolewa na NMB kwa kushirikiana na LAPF ambapo sifa ya kwanza ya kupata mkopo huu ni kuwa na akaunti ya NMB pamoja na kuwa mwanachama wa mfuko wa LAPF na mwanachama awe ameshachangia angalau mara tatu (miezi mitatu).

NMB imetambua changamoto ambazo mfanyakazi anazipata pale tu anapoanza kazi mpya hivyo mkopo wa Anza Maisha utawanufaisha wanachama wa mfuko wa LAPF kujiendeleza pale walipokwama kwasababu ya kukosa fedha za kuanzia maisha.

Mkopo wa Anza Maisha ulitambulishwa rasmi kwenye mkutano mkuu wa 8 wa mwaka wa wanachama wa LAPF uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Leave A Reply